Breaking News

DOG NEWS

Aina Kumi za Mbwa unaopaswa kuwajua

Kama ilivyo kawaida kwa Binadamu kuwa na makabila au race basi vivyo hivyo Kwa Wanyama kama Mbwa napo kuna breed zaidi ya 150 na kila kabila na tabia zake. Leo tunaangalia Makabila matano ya Mbwa ambayo ni :-
1: Affenpinscher
Aina hii ya Mbwa inaitwa Affenpinscher ni aina flani hivi ya mbwa ambao hupatikana sana ndani ya Nyumba za watu ambao wanapenda kampani ya mnyama huyu.Aina huwa na Umbo dogo kama ambavyo anaonekana katika picha

2:Germany Shepherd Dog
Aina hii ya Germany Shepherd imekuwa maarufu sehemu mbalimbali za dunia hususani Tanzania ambapo wengi wanawafahamu hawa mbwa kama Mbwa wanaotumiwa na Jeshi la Polisi kitengo cha Mbwa. Mbwa hawa asili yao ni Ujerumani. 

3: BoerBoel:
Aina hii inajulikana kwa jina la BoerBoel ambapo asili ya Mbwa hawa ni huko Afrika Kusini, Mbwa huyu anamuonekano unaotaka kufanana na simba, na ni aina flani ya mbwa ambae ana umbo kubwa na lenye mvuto. Siku zijazo tutamuangalia kwa Undani zaidi.
4: Doberman Pinscher
 Mbwa huyu anaitwa Doberman Pinscher ambae asili yake ni Ujerumani pia Lakini mbwa huyu inasemekana ni moja kati ya mbwa hatari sana.
5:Rottweiller
Huyu anaitwa Rottweiller ambae pia asili yake ni huko Ujerumani, Mbwa huyu kwa Tanzania anafahamika kama Macho manne kutokana na vidoti viwili alivyonavyo juu ya macho yake. Ni mbwa mmoja mzuri sana lakini anayehitaji uangalizi wa hali ya juu 
6:Belgian Mallinois
Mbwa huyu anaitwa Belgian Mallinois ambae asili yake ni nchini Ubeligiji Mbwa huyu anatumika sana na Majeshi katika Nchi mbalimbali kama vile Ujerumani, Marekani na kwingineko, Huku kwetu hajaweza kuwa maarufu sana lakini pia wengi hawamfahamu na wakimuona basi umfananisha na Germany shepherd na kumpa jina hilo ilhali sio kweli.
7:Maltesse
Aina hii inaitwa Maltesse ambapo kwetu Tanzania hupenda kusema mbwa wa mapambo ambae wengi husema huyu kazi yake sio kulinda
8:Great Dane
Huyu ndio Great Dane mbwa hawa wameanza kushika hatamu katika nchi yetu ya Tanzania ambapo sasa wafugaji wengi wameanza kuwa nao kutokana na Umahiri wake katika nyanja mbalimbali kama ulinzi
9:Cane Corso
Huyu anaitwa Cane Corso ukimuangalia vibaya unaweza sema ni BoerBoel kumbe sio Huyu asili yake ni Nchini Italia. Siku za mbele tutamuangalia kwa undani zaidi Endelea kuwa nasi

10:American Pit Bull Terrier
Anaitwa American Pit Bull Terrier mbwa huyu inasemekana ndio mbwa hatari kabisa kuliko mbwa aina nyingine lakini bado kuna mijadala mingi inayosema kuwa mbwa huyu ni hatari zaidi kuliko wengine huku wengine wakisema sio.Picha zote kwa hisani ya Mtandao.

Tutaendelea kuangalia aina nyingine ya mbwa kwa Leo tuishie hapa 

No comments