Je upo tayari Kumiliki Mbwa Nyumbani Kwako?
Kabla ya kutaka kuleta mbwa nyumbani kwako ni muhimu kujichunguza kama mbwa ni sahihi kwako na familia yako. Kwa maana ya kuwa Kufuga mbwa inaweza kuhitaji uzoefu na kujitoa kwa hali ya juu sana katika kuhakikisha mbwa huyo anapata matunzo sahihi pindi umletapo nyumbani kwako. Fahamu ya kuwa kabla hujapeleka mbwa nyumbani Kwako kwanza Jiulize Maswali yafutayo lakini swali kuu na moja ambalo unapaswa kujiuliza ni hili Kwanini unahitaji Mbwa Nyumbani Kwako?
1: Je napenda kweli mbwa?
Kupenda kitu kunakufanya uweze kuhudumia kitu hiko hata kama kitaleta usumbufu usitakiwa kwa muda flani na kwa kupenda huko ndio kutakufanya usumbufu ule usione kama ni usumbufu bali utaweza kuwa na amani katika kuhudumia kitu hiko.
Fahamu kuwa uamuapo kufuga mbwa basi unatakiwa ufahamu kuwa Unaongeza mwanafamilia Mpya ndani ya familia yako ambae atakutegemea kwa kila kitu kwa muda wa zaidi ya miaka 10 mpaka 15. Kama unaona huna mapenzi na mbwa nakushauri usifuge maana utaona ni usumbufu kwako na hatimaye utashindwa kumuhudumia na muda mwingine utaweza kusababisha matatizo kwa familia yako au hata jamii yako.
2:Je Upo tayari kumuhudumia katika maisha yake yote ikiwa pamoja na kumpa muda wako?
Ukijiuliza swali hili kisha ukajipa jibu kuwa NDIO nipo tayari basi fahamu kuwa utatakiwa kutimiza wajibu wako katika kuhakikisha mwanafamilia wako huyo mpya unamuhudimia ikiwa pamoja na kumpa muda wako. Ukijiona haupo tayari basi fahamu kuwa hutoweza kufuga mbwa na nakushauri achana na hilo wazo.
3:Una Muda wa kumuonyesha Mapenzi Mbwa wako?
Kufuga mbwa sio kama kufuga kuku au bata, Kufuga Mbwa ni tofauti na kufuga kuku au bata ambapo Mbwa ukimfuga ni lazima umuonyeshe mapenzi yako kwake ili na yeye akupe mapenzi yake kwako. Ukishindwa Kumpa mapenzi yako fahamu naye hawezi kukupa mapenzi kwasababu yeye hufamu kabisa mtu anayempenda na asiyependa na madhara yake akifahamu kuwa huna mapenzi naye basi hatokupenda na anaweza kukuchukia na kukuona adui kwake na pengine kusababisha madhara kwako. Kama huna muda basi ni heri usifuge mbwa kwasababu utapata shida wewe.
Kuna sababu nyingi sana zinazosababisha Mtu au watu kufuga Mbwa nyumbani kwao. Na hizi ni baadhi tu ya sababu hizo chache za kwanini Mtu uhitaji kufuga mbwa.
The Good
1:Kampani - Watu wengi hufuga mbwa kwasabau tu yakuwapa kampani katika mambo yao kama vile kutembea jioni, Kwenda kwenye fukwe za bahari na sehemu mbalimbali lakini pia Mbwa wamekuwa sehemu kubwa sana ya maisha ya binadamu kwasababu mbwa ndio rafiki pekee ambaye ukimuonyesha mapenzi basi yeye atarudisha mara mbili yake.
2:Afya- Kufuga mbwa ni sehemu moja wapo ya muhusika kuwa na afya njema kutokana na kutoa muda wake mwingi kuhakikisha anamuhudumia mbwa huyo na kumfanya kuwa na shughuli ya kufanya kuliko kukaa bila kuwa na shughuli lakini pia Mbwa amekuwa na mchango mkubwa katika afya ya binadamu kutokana na namna ambavyo atakufanya kuwa busy katika Mambo mbalimbali kama vile michezo, kutembea nae muda wa jioni na kufanya mazoezi pamoja nae.
3:Furaha - Asilimia kubwa ya wanaofuga mbwa na kuwapa muda wa kutosha huwa na furaha kwasababu unapomuhudimia mbwa kutokana na mapenzi uliyo nayo ni dhahiri shahiri kuwa unapohudumia kitu unachopenda ni dhahiri utakifurahia na umfurahiapo mbwa wako Basi ni dhahiri kabisa unaongeza kiwango cha furaha katika maisha yako.
4: Ulinzi - Watu wengi wamekuwa wakihitaji mbwa kwaajili ya kuwapa ulinzi wa mali zao na maeneo yao na hii imekuwa sababu kubwa sana na hitaji kubwa sana kwa watu wengi kutaka kuwa na mbwa japokuwa sio mbwa wote wanaweza kuwa ni waulinzi
4: Ulinzi - Watu wengi wamekuwa wakihitaji mbwa kwaajili ya kuwapa ulinzi wa mali zao na maeneo yao na hii imekuwa sababu kubwa sana na hitaji kubwa sana kwa watu wengi kutaka kuwa na mbwa japokuwa sio mbwa wote wanaweza kuwa ni waulinzi
5: Biashara - Siku za hivi karibu nchini Tanzania Mbwa ameanza kuwa sehemu ya kuingiza kipato kutokana na biashara yake kushamiri kutokana na uelewa wa watu kukua kuhusiana na mbwa. Mbwa anaweza kuuzwa mpaka shilingi Milioni Mbili za Kitanzania, Kwahiyo kufuga mbwa pia ni biashara ambayo huongeza kipato chako wewe mwenyewe mbwa.
JE UPO TAYARI KUISHI NA MBWA?
Kuishi na mbwa ni gharama kwasababu mbwa anahitaji matunzo, chakula, mafunzo na vifaa vya michezo. Kama wewe unaona kabisa kuwa huna uwezo wa kumuhudimia mbwa ni heri usiamue kuwa nae kwasababu mbwa anahitaji kutibiwa na kupewa chanjo kila baada ya muda, anahitaji kupelekwa kwa daktari wa mifugo kwaajili ya uchunguzi na vitu vingine kama hivyo pindi awapo mzima au anaumwa sasa kama huna uwezo maana yake ni kwamba Mbwa huyo utashindwa kumuhudumia na atimaye anaweza kupoteza maisha
JE UPO TAYARI KUWA MUWAJIBIKAJI KWA MBWA WAKO?
Unapofuga mbwa fahamu kuwa lazima uwajibike kwake katika kipindi chote cha maisha yake.
Kwasababu Mbwa huitaji vitu vingi sana kama vile
1:Mbwa anahitaji kupelekwa kufanyiwa uchunguzi na na kupewa chanjo kila mara
2: Mbwa anahitaji kulindwa dhidi ya minyoo na bacteria wakila aina
3:Mbwa anahitaji usafi wa hali ya juu kuanzia sehemu anayolala na vyombo vyake vya kulia chakula.
4:Mbwa anahitaji kufundishwa kutokana na mazingira aliyopo
5:Mbwa anahitaji kupewa mazoezi kwaajili ya Kulinda afya yake.
Je upo tayari kufanya hayo yote?Jitathimini
No comments