Breaking News

DOG NEWS

Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Pili

Picha/Makala na Josephat Lukaza
Siku ya Leo tutaangalia Makundi mawili yaliyobaki katika makundi mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa, Siku zilizopita Katika makala ya Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Kwanza tuliweza kuangalia Makundi mawili ambayo ni Viral Infections pamoja na Bacterial Infections. Leo tutaangalia makundi mengine mawili ya mwisho ambapo tutapata nafasi ya kuangalia ni magonjwa gani yapo katika Makundi hayo mawili yaliyosalia.

Yes Let's Back to Class kama wasemavyo Wazungu, Leo tutaangalia Makundi Mengine Mawili ambayo ni Kama Ifuatavyo

1: Fungal Infections
Fungal infections ni magonjwa ambayo  husababishwa na fangasi magonjwa haya yanaathiri binadamu pamoja na mbwa japokuwa Mbwa hushambuliwa mara kumi zaidi ya binadamu kwa magonjwa yasababishwyo na fangasi. Magonjwa yasababishwayo na fangasi kwa Mbwa yanaweza kuleta madhara katika Macho, Ubongo, ngozi nk. Katika Kundi hili la magonjwa yasababishwayo na fangasi Ni kama vile Blastomycosis, Histoplasmosis,Coccidioidomycosis,Cryptococcosis,Ringworm,Sporotrichosis,Aspergillosis, Pythiosis pamoja na Mucormycosis.

Katika kundi hili kuna magonjwa baadhi ambayo binadamu anaweza kuyapata na kuathirika na mbwa pia akayapata na kuathirika kama vile Cryptococcosis, Blastomycosis nk. Kundi la Pili Ni

2: Protozoal diseases
Haya ni baadhi ya magonjwa ambayo yapo katika kundi hili, Magonjwa haya asilimia kubwa humuathiri Mbwa na kupelekea kuharisha na muda mwingine kupiteza uzito kwa haraka sana baadhi ya magonjwa hayo katika kundi hili ni kama vile Giardiasis, Coccidiosis, Leishmaniasis, Babesiosis, Protothecosis pamoja na Neosporosis

Kwa leo tumemalizia Makundi mengine mawili ambayo hufanya makundi haya kuwa Manne, Endelea kutembea Blogu yetu kwa Taarifa mbalimbali zinazohusu ufugaji bora na wa kisasa wa Mbwa.

Kwa Maoni na ushauri basi usisite kutuandikia katika sehemu ya komenti huku ukiacha mawasiliano yako ya barua pepe endapo ungependa kupokea feedback au majibu ya Maoni au ushauri wako au maswali yako.

Dog Tips Tanzania For Better Keeping of Your Dogs

2 comments:

  1. Kuna ugonjwa ambao mbwa anavimba sehem ya chini kalib na chuchu huu upo kundi gan na nn tiba make

    ReplyDelete
  2. Nini tiba ya ugonjwa namba mbili?

    ReplyDelete