Mbwa Rafiki wa Binadamu
Picha kwa Hisani ya Josephat Lukaza
Mbwa ni mmoja ya wanyama rafiki wa binadamu tokea enzi na enzi , Siku za Hivi karibuni nchini Kwetu Tanzania Watu wengi wameanza kuwa na uelewa na ufahamu wa Mbwa na kuanza kuwathamini na ukizingatia Mbwa amekuwa msaada mkubwa sana katika shughuli mbalimbali kama ulinzi, ufuatiliaji na mambo mengine.
Aina za Mbwa zipo nyingi sana lakin kwa nchi yetu baadhi ya mbwa wameonekana kwa wingi kama Germany Shepherd ambao watu wengi wakiona mbwa utasikia Mbwa Wa Polisi, Rottyweiller, DoberMan, BoerBoel, nk. Hawa ni baadhi ya mbwa ambao kwa asilimia kubwa wanapatikana ndani ya nchi yetu kwa asilimia kubwa.
Mbwa amekuwa rafiki mzuri sana kwa binadamu, na pia amekuwa Mmoja kati ya wanyama ambao wakifundishwa basi wanafundishika kisawasawa lakini angalizo ni kuwa Mnyama anabaki kuwa mnyama tu.
Ushauri wangu tuwapende Mbwa, tuwatunze maana mbwa akiwa rafiki yako basi ana faida kubwa sana ambapo hata wewe ukiwa katika hali ya stress fika mbwa wako atakuwa sehemu ya kukufariji maana mbwa anafahamu kabisa kuwa bosi wake leo hayuko sawa.
Kwa mahitaji ya Mbwa wasiliana na sisi kwa ushauri na mambo mengi usisite kuwasiliana nasi
No comments